Makundi ya waasi nchini Syria yamepokea shehena mpya ya tani 35 za silaha kutoka serikali ya Saudi Arabia. Salim Idriss mmoja kati ya viongozi wa Baraza la Kijeshi la kundi la waasi liitwalo 'Jeshi Huru la Syria' kutoka Amman nchini Jordan kwamba, kundi hilo limepokea silaha mpya kutoka Saudi Arabia kwa shabaha ya kupambana na majeshi ya serikali ya Syria.
Gazeti la Washington Post limeandika kuwa, Salim Idriss pia ameitaka serikali ya Marekani iwapatie kuanzia mwezi ujao waasi hao wa Syria kila wiki tani 700 za silaha na zana za kijeshi. Hivi karibuni Robert Stephen Ford balozi wa zamani wa Marekani nchini Syria alifanya safari katika eneo la mpaka wa Syria na Uturuki na kusambaza shehena za silaha kwa makundi ya waasi nchini Syria.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO