Rais Barack Obama wa Marekani atakutana na waziri mkuu wa Uingereza katika Ikulu ya Marekani siku ya Jumatatu kujadili suala la Syria na mkutano ujao wa kundi la mataifa majiri yenye viwanda ya G8 mwezi ujao , mkutano utakaofanyika nchini Ireland ya kaskazini.
Taarifa ya Ikulu ya Marekani, ya White House, imesema kuwa ziara ya waziri mkuu wa Uingereza inaonyesha uhusiano maalum kati ya Marekani na Uingereza , uhusiano ambao umekuwa muhimu katika kuendeleza usalama wa mataifa hayo pamoja na ufanisi.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa pamoja na suala la Syria na G8, mazungumzo hayo pia yatajumuisha masuala ya biashara na ushirikiano wa kiuchumi na mapambano dhidi ya ugaidi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO