Umoja wa Mataifa umesema kuwa sera za kibaguzi za Israel zimesababisha asilimia 80 ya watoto wa Kipalestina kuishi katika umasikini huko mashariki mwa mji wa Quds.
Hayo yameelezwa katika taarifa ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo (UNCTAD) na kwamba umasikini wa Wapalestina katika mji wa Quds umeongezeka katika muongo uliopita. UNCTAD pia imetoa wito wa kuhitimishwa shughuli za ujenzi usio halali wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina na imekosoa ujenzi wa uzio wa kibaguzi katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mato Jordan unaokaliwa kwa mabavu na Israel.
Wakati huo huo askari wa utawala wa Kizayuni wamewapiga Wapalestina walikuwa wamejikusanya nje wa Msikiti wa al Aqsa huko mashariki mwa Quds na kuwakamata makumi ya vijana wa Kipalestina.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO