Chama kilichopigwa marufuku cha Wafanyakazi wa Kurdistan (PKK) wanaopigania kujitenga kwa jimbo hilo leo wameanza kuwaondowa wapiganaji wake kutoka Uturuki na kuwapeleka kaskazini mwa Iraq. Msemaji wa chama cha Amani na Demokarasi cha Wakurdi amesema kwamba mchakato huo umeanza kutekelezwa na hivyo ndivyo wanavyofahamu hata hivyo chama hicho hakikutowa ufafanuzi zaidi. Hapo mwezi wa Machi kiongozi wa chama hicho cha PKK alieko gerezani Abdullah Ocalan alitowa wito wa kusitishwa kwa mapigano kama msingi wa kufikia suluhisho la kisiasa katika mzozo huo wa miongo mitatu kuhusiana na haki za Wakurdi nchini Uturuki.
Pande zote mbili hapo jana zimeonya dhidi ya vitendo vya uchokozi. Uongozi wa PKK umesema kwamba nyendo za vikosi vya Uturuki na matumizi ya ndege zisisizo na rubani kwa ajili ya uchunguzi ni mambo ambayo yanakwamisha kuondolewa kwa wapiganaji hao.Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametaka wapiganaji hao wa PKK waondoke bila ya silaha kwa kuziacha silaha hizo nchini Uturuki.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO