Sunday, May 12, 2013

SYRIA YAKANUSHA KUHUSIKA NA MASHAMBULIZI YA UTURUKI


Serikali ya Syria imekanusha madai kwamba imehusika na miripuko ya magari yaliyokuwa yametegwa mabomu kwenye mji wa mpakani wa Teyhanli nchini Uturuki na ambayo yamepelekea watu 46 kuuawa.
Waziri wa Habari wa Syria, Omran az Zohbi amewaambia waandishi wa habari leo Jumapili kuwa nchi yake haikufanya na wala haiwezi kufanya kamwe mashambulizi kama hayo kwani misingi ya serikali hiyo hairuhusu kufanya hivyo.
Waziri huyo wa Syria amewalaumu viongozi wa Uturuki kuhusiana na mashambulizi hayo ya jana Jumamosi na vile vile kwa kuhusika kwao moja kwa moja na machafuko yanayoendelea nchini Syria na kwa kuruhusu magaidi watumie mpaka wa Uturuki kuingiza silaha, miripuko, magari ya kijeshi, wanamgambo na fedha ili kufanya mauaji ya raia ndani ya ardhi ya Syria.
Waziri wa Habari wa Syria amesema: "Ni Erdogan, (Waziri Mkuu wa Uturuki) ndiye anayepaswa kuulizwa kuhusu mashambulizi hayo. Yeye na chama chake ndio wanaobeba jukumu la moja kwa moja la mashambulio hayo." Mwisho wa kunukuu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO