Sunday, May 12, 2013

VITUO VYA POLISI VYASHAMBULIWA BENGHAZI


Vituo viwili vya polisi vimeshambuliwa katika mji wa mashariki wa Libya wa Benghazi mapema leo asubuhi baada ya kushambuliwa kwa vituo vyengine viwili na mabomu hapo Ijumaa.
Shambulio hilo ni ishara ya karibuni ya ukosefu wa utulivu katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Libya mahala ambapo ndiko lilikoanzia vuguvugu lililompindua dikteta Muammar Gaddafi hapo mwaka 2011.Takriban miaka miwili kufuatia kupinduliwa kwake makundi ya upinzani ambayo yalisaidia kumpinduwa bado yanagoma kuvunjwa na yamekuwa yakionekana zaidi mitaani kuliko hata vikosi vya usalama.Msemaji wa Baraza la serikali ya mitaa la Benghazi Osama bin Sharif amesema hawaridhishwi na utendaji wa wizara ya mambo ya ndani na hususan uongozi wa polisi wa Benghazi.Wiki hii wanadiplomasia walianza kuondoka mji mkuu wa Tripoli ambapo hali ya usalama ilizidi kuwa mbaya mwishoni mwa mwezi wa Aprili wakati wanamgambo wenye silaha walipozitwaa wizara mbili za serikali kushinikiza madai yao kupitishwa na bunge.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO