Ndege za kivita za Ufaransa zimeendelea kudondosha mabomu katika eneo la kaskazini mwa Mali. Duru zinaarifu kuwa ndege hizo za kivita za Ufaransa zimelenga ngome za waasi wenye misimamo mikali wa kundi linalojiita Ansar Din katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Hayo yanajiri katika hali ambayo Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amesema wanajeshi wa nchi yake watabakia Mali kwa muda usiojulikana. Ufaransa ilikuwa imeahidi kuwa itawaondoa wanajeshi wake wote Mali mwezi uliopita wa Aprili. Wakati huo huo afisa wa ngazi za juu katika Jeshi la Mali ameituhumu Ufaransa kuwa inawapendelea waasi wa Tuareg nchini humo. Waasi wa Tuareg wako katika kundi la Azawad linalipigania kujitenga kaskazini mwa Mali.
Ufaransa ilianzisha vita nchini Mali Januari 11 mwaka huu kwa kisingizio cha kukabiliana na waasi eneo la kaskazini mwa nchi hiyo. Weledi wa mambo wanasema lengo kuu la hujuma ya Ufaransa huko Mali ni kupora utajiri wa nchi hiyo hasa mafuta ya petroli, dhahabu na madini ya urani.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO