Sunday, May 19, 2013

WATURUKI WAPINGA KUUNGWA MKONO WAASI SYRIA


Wananchi wa Uturuki wameandamana katika mji mkuu Ankara kupinga uungaji mkono wa serikali ya nchi yao kwa waasi wa Syria. Katika maandamano hayo polisi waliwatawanja waandamanaji kwa gesi za kutoa machozi ambapo watu kadhaa walijeruhiwa. Waandamanaji hao walikuwa wakitoa nara dhidi ya chama tawala cha Uadilifu na Maendeleo cha Waziri Mkuu wa Uturuki Racep Tayyip Erdogan.
 Hasira za wananchi wa Uturuki zimezidi kushuhudiwa dhidi ya serikali yao inawayounga mkono wapinzani wa Syria, hasa baada ya kutokea milipuko miwili ya kigaidi katika mji wa Reyhanli kusini mwa nchi hiyo tarehe 11 Machi ambapo watu 50 waliuawa. Hapo jana pia polisi walipambana na waandamanaji wenye hasira katika mji huo waliokuwa wakiandamana kuikosoa serikali kwa kushindwa kuimarisha usalama kwenye mji huo. Maandamano kama hayo yalishuhudiwa pia katika mji wa Antakya. 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO