Wednesday, May 15, 2013

UN KUPIGIA KURA AZIMIO JUU YA SYRIA

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupigia kura rasimu ya azimio linalohusiana na mgogoro wa Syria. Rasimu hiyo iliyoandaliwa na Qatar kwa ushirikiano wa baadhi ya nchi za Kiarabu inalenga kukemea serikali ya Syria kwa kile kinachodaiwa eti ni kukiuka haki za binadamu. Hata hivyo Rusia ambayo ni mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imesema inapinga vikali rasimu hiyo ambayo imesema ina malengo ya kisiasa. Mwanadiplomasia mmoja wa UN ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema nchi nyingi huenda zikakosa kupiga kura kutokana na kutoikubali rasimu hiyo. Mwanadiplomasia huyo amesema kuwa, makundi ya kigaidi kama vile al-Qaeda ambayo yametangaza wazi kuweko kwao huko Syria hayajakemewa kwenye rasimu hiyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO