Shirika la Ujasusi la Marekani CIA limetangaza kuwa, asilimia 75 ya wananchi wa Syria watamchagua Rais Bashar Assad kwenye uchaguzi wa rais utakaofanyika mwaka 2014. Taarifa iliyotolewa na Shirika la Ujasusi la Marekani imeeleza kuwa, kama Rais Assad atajitosa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi wa rais hapo mwakani, bila shaka ataibuka mshindi na kuiongoza tena nchi hiyo hadi mwaka 2020. Uchunguzi wa maoni uliofanywa na shirika hilo la kijasusi ndani ya Syria unaonyesha kuwa, Rais Assad bado ana uungaji mkono mkubwa wa wananchi wa nchi hiyo. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, machafuko na mapigano yanayoendelea nchini humo yanaonyesha kuimarika zaidi nguvu za kijeshi za nchi hiyo dhidi ya makundi ya kigaidi, na huenda mapigano hayo yakaendelea hadi wakati wa kufanyika uchaguzi wa rais nchini humo. Inafaa kuashiria hapa kuwa, nchi za Magharibi na hasa Marekani na Uingereza, pamoja na nchi waitifaki za Saudi Arabia, Qatar na Uturuki zimekuwa mstari wa mbele katika kuyapa misaada ya kifedha na kisilaha makundi ya kigaidi nchini Syria, kwa shabaha ya kuuangusha utawala uliochaguliwa na wananchi wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO