Monday, May 20, 2013

WAISLAM NIGERIA WAPINGA MARUFUKU YA KUVAA HIJAB

Waislamu nchini Nigeria wamelaani marufuku ya vazi la hijabu katika shule za serikali nchini humo. Ripoti iliyotolewa na Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Vyuo Vikuu vya Serikali (Obafemi Awolowo) nchini, imelaani vikali tangazo la kupiga marufuku vazi takatifu la hijabu katika shule zote za Lagos na kuitaja marufuku hiyo kuwa ni mwanzo wa kukanyagwa haki za wanafunzi wa Kiislamu nchini humo. Aidha Waislamu nchini Nigeria wamelalamikia hatua hiyo na kuwataka viongozi wa Lagos kufuta mara moja marufuku hiyo. Kwa upande mwingine Waislamu hao wametoa wito kwa serikali ya Lagos kulaani hatua ya kuwasajili wanafunzi wanaovaa hijabu mashuleni na kuongeza kuwa, serikali inapaswa kufahamu kuwa, uendeshwaji wa shule za serikali unatokana na kodi zao na kwamba, ni haki yao kunufaika na shule hizo bila kubaguliwa kiimani. Wakati huo huo Msemaji wa serikali ya Nigeria Reuben Abati amesema kuwa, Rais Goodluck Jonathan wa nchi hiyo amelitaka kundi lenye misimamo mikali la Boko Haram kuweka chini silaha na kurudi kwenye meza ya mazungumzo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO