Sunday, May 19, 2013

WAISLAM WAONGEREZA NCHINI UINGEREZA

Vyombo vya habari nchini Uingereza vimetangaza juu ya kuongezeka idadi ya Waislamu, huku idadi ya Wakristo ikizidi kupungua kwa kasi nchini humo. Toleo la jana Jumamosi la gazeti la Independent limeandika kuwa, pamoja na kuwepo propaganda chafu dhidi ya Waislamu nchini Uingereza, lakini idadi ya Waislamu nchini humo inazidi kuongezeka siku hadi siku huku idadi ya Wakristo ikipungua kwa kasi. Kituo cha Takwimu nchini Uingereza kimetangaza kuwa, idadi ya Wakristo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ilikuwa asilimia 71.7, amma hadi kufikia mwaka 2011 idadi hiyo ilipungua na kufikia asilimia 59.3. Gazeti hilo limeandika kuwa, miongoni ma sababu za vijana wa Kiingereza kuvutiwa na dini ya Kiislamu ni upendo unaoonyeshwa na wafuasi wa dini ya Kiislamu nchini humo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO