Wananchi wa Libya walifanyika maandamano hapo jana Ijumaa mjini Tripoli, kuishinikiza serikali ya nchi hiyo kuchukua hatua za haraka kuunda jeshi la polisi na usalama wa taifa. Maandamano hayo yaliyoandaliwa na taasisi za kijamii nchini Libya, yalifanyika mji mkuu Tripoli ambapo waandamanaji walipiga nara zilizokuwa na jumbe wa kutaka kuundwa jeshi la polisi na lile la kujenga taifa kwa minajili ya kudhamini usalama wa raia, kulinda hali ya amani, kutekelezwa kwa sheria za kijamii na kulinda usalama wa taifa. Aidha kutoa nafasi kwa vyombo vya mahakama nchini humo ili viweze kufanya kazi zake, ni miongoni mwa matakwa ya waandamanaji hao. Maandamano hayo yamefanyika katika hali ambayo wiki iliyopita makumi ya watu waliuawa na kujeruhiwa kufuatia mlipuko wa bomu uliotokea huko mjini Bengazi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO