Saturday, May 18, 2013

ASKARI BAHRAIN YAWATIA MBARONI WATU 300

Kiongozi wa kituo cha kutetea haki za binaadamu nchini Bahrain amesema kuwa, karibu wanaharakati 300 nchini humo wametiwa mbaroni na askari wa utawala wa Aal Khalifa. Abbas Imran kiongozi wa kituo hicho ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na televisheni ya Kiarabu ya Al-Alam na kuongeza kuwa, hali ya wanaharakati wengine wa kisiasa akiwemo Abdul-Wahhabi Hussein na Hassan Mushamma’a ambao wanaendelea kushikiliwa katika jela za utawala huo ni mbaya sana. Amesema hatua ya askari wa utawala wa Aal Khalifa ya kuendelea na kamata kamata yao dhidi ya raia na wanaharakati wa kutetea haki za binaadamu nchini humo akiwamo Naji Fatil na Hisham as-Sabagh, inadhihirisha wazi ni namna gani utawala huo ulivyokuwa wa kimabavu na unaokanyaga haki za raia wa nchi hiyo. Aidha Imran amesisitiza kuwa, utawala wa Bahrain unavunja wazi sheria za kimataifa kwa kuwashambulia wananchi wanaofanya maandamano ya amani kupinga utawala huo.  

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO