Waandamanaji nchini Libya wamechoma moto bendera ya Qatar huko mjini Tobruk magharibi mwa nchi hiyo, kutokana na kile walichosema kuwa ni uingiliaji wa serikali ya Doha nchini mwao. Waandamanaji hao walipiga nara wakiitaja Qatar kuwa chanzo cha ukosefu wa amani na uthabiti wa kisiasa nchini Libya na kuitaka serikali ya sasa ya Tripoli kufanya juhudi kubwa za kuzima njama hizo za Qatar nchini humo. Aidha maandamano hayo yaliyowajumuisha pia wanasiasa na wanaharakati wa nchi hiyo, yaliituhumu Qatar kuwa, inatumia uwezo wake wa kifedha katika kuyaunga mkono makundi ya wabeba silaha wanaofelisha juhudi za kuundwa serikali yenye nguvu nchini Libya. Viongozi wengi wa Tripoli wanaamini kuwa, hatari kubwa inayoikabili Libya hivi sasa ni uingiliaji wa Qatar nchi humo kwa kutumia makundi ya wanamgambo wenye misimamo mikali na wanaofungamana na kundi la kigaidi la Al-Qaida kwa minajili ya kulidhibiti eneo la kaskazini mwa Afrika.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO