Monday, May 13, 2013

WATURUKI WAANDAMANA KUPINGA MAANDAMANO SERIKALI YA NCHI HIYO

Mamia ya Waturuki wamefanya maandamano katika mji wa Antakya, wakipinga siasa zinazotekelezwa na serikali ya Ankara. Washiriki wa maandamano hayo yaliyojiri katika mji wa Antakya kusini mwa Uturuki, wameilani serikali ya Ankara na kuitaja kuwa muhusika wa miripuko ya hivi karibuni katika mji wa mpakani wa Teyhanli nchini humo. Kabla ya hapo pia wananchi wa mji wa Teyhanli walimtaka Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ajiuzulu wadhifa wake kutokana na milipuko hiyo. Hii ni katika hali ambayo Waziri wa Habari wa Syria, Omran az Zohbi jana aliwambia waandishi wa habari kuwa, nchi yake haikuhusika na wala haiwezi kufanya mashambulizi kama hayo kwani misingi ya serikali ya Damascus haiyaruhusu. Omran pia amewalaumu viongozi wa Uturuki kuhusiana na mashambulizi hayo ya juzi Jumamosi na vile vile kwa kuhusika kwao moja kwa moja na machafuko yanayoendelea nchini Syria na kwa kuruhusu magaidi watumie mpaka wa Uturuki kuingiza silaha, miripuko, magari ya kijeshi, wanamgambo na fedha ili kufanya mauaji ya raia katika ardhi ya Syria. Miripuko ya magari yaliyokuwa yametegwa mabomu kwenye mji wa mpakani wa Teyhanli nchini Uturuki yamepelekea watu 46 kuuawa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO