Wanawake wawili wamefungwa jela katika jimbo la Minnesota Marekani kwa kosa la kuwatumia fedha waasi wa al-Shabab nchini Somalia.
Amina Farah Ali mwenye umri wa miaka 36 na Hawo Mohammad Hassan mwenye umri wa miaka 66 ambao ni raia ya Marekani wamehukumiwa kifungo cha miaka 10 kila mmoja kwa madai ya kujihusisha na kile kinachodaiwa ni ugaidi na vile vile kuwadanganya makachero wa Shirika la Upelelezi la Marekani FBI.
Wawili hao wamekanusha madai hayo na kusema walikuwa wakituma fedha Somalia kuwasaidia watu masikini katika nchi hiyo walikozaliwa. Mawakili wa wanawake hao wamesisitiza kuwa walikuwa wakijihusisha na shughuli za kibinaadamu za kuwasaidia mayatima na watu masikini. Aidha wamesema walikuwa wakiwatumia pesa wale ambao walikuwa wakipambana dhidi ya vikosi vamizi vya kigeni Somalia wakati nchi hiyo ilipokuwa imekaliwa kwa mabavu na Ethiopia kati ya mwaka 2006-2009. Wananchi wengi wa Somalia walivitazama vikosi vya Ethiopia kama vikosi vamizi vilivyokuwa nchini humo kinyume cha sheria chini ya himaya ya Marekani.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO