Russia imesema Shirika la Kijasusi la Marekani CIA 'limevuka mstari mwekundu' kwa kupuuza onyo la Moscow kuhusu njama zake za kujaribu kuwashawishi wafanyakazi wa mashirika ya usalama ya Russia kuhudumia CIA kama majasusi.
Msemaji wa Shirika la Usalama la Russia (FSB) Nikolai Zakharov amesema kuwa Oktoba mwaka 2011 FSB iliionya rasmi CIA kuacha njama zake za kutafuta majasusi Russia.
Mei 14 maafisa wa usalama Russia walimtia mbaroni mwanadiplomasia wa Marekani aliyetambuliwa kama Ryan Fogle kwa kosa la kujaribu kumshawishi raia wa Russia ahudumu kama jasusi wa CIA. Fogle aliachiliwa huru na kuamuriwa kuondoka Russia mara moja.
Mara kwa mara maafisa wa usalama wa Russia wamekuwa wakiwanasa wanadiplomasia wa ubalozi wa Marekani mjini Moscow wanaojihusisha na vitendo vya kijasusi kinyume na kanuni za kidiplomasia.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO