Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran Saeed Jalili na Mkuu wa Sera za Kigeni Umoja wa Ulaya Catherine Ashton wamemaliza mkutano wa Istanbul, Uturuki.
Akizungumza na waandishi habari, Jalili amesema mazungumzo yake na Ashton ‘yamezaa matunda’ na kwamba watakutana tena katika mustakabali wa karibu.
Ashton ambaye anawakilisha nchi za 5+1 ambazo ni Uchina, Ufaransa, Russia, Uingereza, Marekani na Ujerumani amesema mazungumzo yake na Jalili yalikuwa ‘yenye manufaa’. Amesema baada ya mazungumzo hayo ya Mei 15 watatafakari kuhusu hatua itakayofuata katika mchakato huo.
Kabla ya kikao hicho, Jalili alisema Iran ingali inasubiri jibu kuhusu mapendekezo iliyotoa katika kikao chake na 5+1 huko Almaty Kazakhstan mwezi Aprili.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO