Thursday, May 16, 2013

NIGERIA YAANZA KUPAMBANA NA NA BOKO HARAM


Jeshi la Nigeria Jumatano lilianzisha oparesheni kali ya kuwakamata wanamgambo wa Boko Haram walio mafichoni kufuatia amri ya Rais Goodluck Jonathan ambaye ametangaza hali ya hatari katika majimbo matatu ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Imearifiwa kuwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Nigeria wanatekeleza oparesheni kubwa ya kuangamiza waasi wa Boko Haram na kuchukua udhibiti wa maeneo yanayoshikiliwa na waasi hao. Oparesheni hiyo inatekelezwa katika majimbo ya Borno, Adamawa na Yobe ambayo ni kati ya maeneo masikini zaidi nchini Nigeria. Boko Haram ni kundi lenye misimamo ya kufurutu mipaka nchini Nigeria ambalo kutokana na kuwa na ufahamu mbaya na potofu kuhusiana na Uislamu, limeitumbukiza nchi hiyo katika dimbwi la machafuko na mauaji sambamba na kuzusha hitilafu za kidini na kikabila. Umasikini kwa upande mmoja na upendeleo mkubwa baina ya Wakristo na Waislamu nchini Nigeria kwa upande wa pili ni moja ya sababu zinazotajwa na wataalamu wa mambo kuwa chanzo cha vijana wa nchi hiyo kujiunga na kundi la Boko Haram.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO