Wednesday, May 22, 2013

DRONE ZA MAREKANI ZINAUA RAIA WASIO NA HATIA

Shirika la kimataifa la kufuatilia migogoro (ICG) limetoa ripoti inayosema kuwa, ndege zisizo na rubani za Marekani zimekuwa zikiwaua kwa mabomu raia wa kawaida wasio na hatia nchini Pakistan kinyume na madai ya Washington kwamba ndege hizo zinatumiwa kulenga ngome za makundi ya kigaidi. Shirika hilo lenye makao yake mjini Brussels, Ubelgiji limesema Marekani imeficha ukweli kuhusu mauaji ya raia nchini Pakistan na ameitaka White House kuweka wazi takwimu za raia wasio na hatia waliouawa kutokana na hujuma ya ndege hizo. ICG imesema Marekani imekiuka sheria za kimataifa zinazolinda haki za binadamu na imeutaka Umoja wa Mataifa kuchunguza suala hilo. Marekani inatumia ndege zisizo na rubani katika nchi nyingi duniani ikiwa ni pamoja na Yemen na Somalia.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO