Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle anatarajiwa kufanya ziara rasmi katika maeneo yalioko chini ya Mamlaka ya Wapalestina hii leo. Westerwelle anatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu Salam Fayyad mjini Ramallah. Ziara ya Westerwelle katika Ukingo wa Magharibi inakuja baada ya kukutana na Rais wa Israel Shimon Peres pamoja na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu jana Ijumaa. Waziri huyo wa mambo ya Kigeni wa Ujerumani alielezea uungaji wake mkono juhudi mpya za Marekani za kuanzisha tena mazungumzo yaliyokwama ya amani kati ya Waisrael na Wapalestina.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO