Wednesday, June 19, 2013

BARAZA LA UN KUIJADILI HALI YA LIBYA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili hali ya mambo nchini Libya ambako changamoto za kisiasa na kiusalama zinazoikabili nchi hiyo zimeelezwa kuwa huenda ikawa ni matokeo ya miongo ya uongozi wa kiimla na kutokuwepo taasisi imara za kitaifa.
Hayo yamesemwa na Tarek Mitri, ambaye ni Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya na Mkuu wa Ujumbe wa umoja huo wa kuisaidia Libya, UNSMIL.
Mitri amesema kuwa hali ya hivi sasa Libya inahitaji mdahalo wa kitaifa wa kisiasa, ambao utafikia makubaliano kuhusu masuala yanayopewa kipaumbele katika kipindi cha mpito.
Pamoja na hayo, Bwana Mitri amelifahamisha Baraza la Usalama kuhusu mfumo mzima wa sheria nchini Libya, vikiwemo vifungo vinavyokiuka sheria, hali ya wafungwa nchini Libya na mauaji ya kiholela. Amesema pia kuwa UNSMIL inaendelea kusikitishwa na hali ya wahamiaji na wakimbizi wa ndani nchini Libya, ambayo ni mbovu mno.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO