Wednesday, June 19, 2013

MAWAKILI WA KIISLAM WATAKA OBAMA AKAMATWE

Jumuiya ya Mawakili wa Kiislamu nchini Afrika Kusini imetaka Rais Barack Obama wa Marekani atiwe mbaroni kwa kutenda jinai za kivita.
Jumuiya hiyo ya mawakili imeeleza kuwa, Rais Obama ni mtenda jinai za kivita na wametaka afikishwe kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) iliyoko Uholanzi, baada ya  kutenda jinai za kuwaua wananchi wasio na hatia kwa kutumia ndege zisizo na rubani. 
Makundi mbalimbali ya Waislamu nchini Afrika Kusini yamewataka Waislamu na watetezi wa haki kujitokeza kwa wingi kwenye maandamano ya kulaani siasa za Marekani. Taasisi hiyo imeandaa maandamano makubwa ya kupinga safari itakayofanywa na Rais Obama wiki ijayo nchini humo.  
Rais Barack Obama wa Marekani ataanza safari ya kuzitembelea nchi za Kiafrika za Senegal, Tanzania na Afrika Kusini kuanzia tarehe 26 Juni hadi Julai 3 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO