Mshauri wa Waziri Mkuu wa serikali iliyochaguliwa na wananchi wa Palestina, amesema kuwa, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas), bado ina mahusiano mazuri na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchini Lebanon. Basim Naim ameyasema hayo leo katika mahojiano yake na Shirika la Habari la Lebanon la an-Nashrah na kuongeza kuwa, Harakati ya Hamas itaendelea kushirikiana kwa karibu na kila yule anayeisaidia harakati hiyo kwa namna moja ama nyingine hususan Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Hizbullah. Basim amesisitiza kuwa, harakati ya Hamas haitatoa mwanya kwa adui kuuzorotesha muqawama kwa kuzusha tofauti zinazoweza kuharibu uhusiano wake na Tehran na vilevile Harakati ya Hizbullah. Wakati huo huo, kiongozi wa ngazi za juu wa Harakati hiyo ya Hamas Mahmud Az Zahar amezungumzia kadhia ya Syria na kusisitiza kuwa, kubakia Syria yenye nguvu na kuwepo uhusiano mwema na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Hizbullah ni suala lenye muhimu mkubwa katika eneo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO