Waasi wanaopambana na Vikosi vya Serikali katika Majimbo mawili ya kusini mwa Sudan waridhia kupelekwa kwa misaada ya kibinaadam na dawa kufikia katika maeneo wanayoyadhibiti, Katibu mkuu wa Ofisi inayoshughulikia maswala ya kibinaadam ya Umoja wa Mataifa,Valerie Amos ameeleza. Lakini Muungano wa Waasi wa Sudan uko tayari kukubali kuweka silaha chini baada ya kuwepo kwa mapigano kwa kipindi cha miaka miwili jimboni Kordofani kusini na Blue Nile hivyo Misaada ya kibinaadam inaweza kuwafikia Raia. Umoja wa Mataifa na Mataifa ya Magharibi umesema kuwa mapigano kati ya Waasi wa Sudan People's Liberation Movement-North (SPLM-North) na Jeshi la Sudan vimeleta madhara makubwa katika majimbo hayo hasa huduma za Afya na Chakula.
Umoja wa Mataifa umekadiria kuwa Watu Milioni moja katika majimbo mawili wameathiriwa na Mgogoro na zaidi ya Watu 200,000 wamekimbilia nchi jirani Sudani Kusini na Ethiopia. Valerie Amos amesema Makundi ya Waasi walioko Kordofani na Darfur waliandika waraka wakionesha utayari wao kushirikiana na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuwafikia Raia waliothirika. Maafisa wa Umoja wa Mataifa wana matumaini ya kufanya mazungumzo na Waasi na Serikali mjini Adis Ababa mwezi huu kwa kuanzia mazungumzo hayo yatagusia suala la Chanjo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO