Tuesday, June 11, 2013

MAKAO MAKUU YA NATO YASHAMBULIWA AFGHANISTAN

Wanamgambo nchini Afghanistan wameshambulia makao makuu ya vikosi vya NATO vinavyoongozwa na Marekani nchini humo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kabul. Sauti za milipuko mikubwa na urushianaji risasi zilizikika kwenye eneo hilo ambapo Ayoub Salangi Mkuu wa Polisi wa Kabul amesema, wamewaua watu wote 7 waliofanya mashambulizi hayo. Kundi la Taliban limetangaza kuhusika katika shambulizi hilo na kudai kwamba askari kadhaa wa kigeni wameuawa kwenye shambulio hilo.
Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kabul ni makao makuu ya makamanda wa kikosi cha NATO, na safari zote za ndege za kuingia na kutoka uwanjani hapo zimesimamishwa kutokana na mashambulizi hayo. Vituo vingine vya kijeshi vya NATO katika mji mkuu wa Afghanistan pia vimefungwa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO