Marekani imesema imeilegezea Iran vikwazo vya vifaa vya mawasiliano na kuzifungua huduma za internet na mitandao ya kijamii, kuwasaidia watu wa nchi hiyo kukwepa udhibiti wa serikali.
Hatua hiyo inayapa ruhusa makampuni ya kimarekani kuanza kuuza nchini Iran vifaa kama komputer na simu za mkononi, ambavyo vilikuwa vimesitishwa kutokana na vikwazo kwa nchi hiyo. Makampuni hayo hali kadhalika yataruhusiwa kuwauzia wairan programu za komputer na madishi ya kunasia matangazo kupitia njia ya satelaiti.
Hata hivyo, wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani imesema kuwa vikwazo hivyo vitabakia kwa viongozi wa serikali walio kwenye orodha ya vikwazo. Hatua hiyo ya Marekani imekuja wiki mbili tu kabla ya uchaguzi wa rais nchini Iran. Marekani imeimarisha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran, ikiishutumu nchi hiyo kuwa na mpango wa siri wa kuunda silaha za nyuklia.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO