Saturday, June 01, 2013

SERIKALI YA UTURUKI YAZIDI KUPAMBANA NA WAANDAMANAJI

Recep Tayyip Erdogan, Waziri Mkuu wa Uturuki amesema kwamba serikali haitoacha kuendelea na mpango wake wa kuharibu eneo la bustani, ambao umezusha maandamano makubwa ya kupinga serikali mjini Istanbul na katika miji mingine kadhaa ya nchi hiyo. Erdogan amesema hayo leo huku polisi wakiendelea kuwatawanya waandamanaji wanaopinga serikali kwa kutumia gesi za kutoa machozi mjini Istanbul, waliokuwa wanajaribu kuelekea katika meidani maarufu ya Taksim kwa siku ya pili. Erdogan ameahidi kuendelea na mpango wa kuharibu bustani ya Gezi karibu na meidani hiyo na badala yake kujenga maduka.  Hata hivyo Rais Abdullah Gul wa Uturuki amesema maandamano hayo yamefikia katika hali mbaya na kutoa wito wa kutafutwa suluhisho la kuyahatimisha. Bustani ya Gezi imezoeleka kuwa eneo la mijumuiko, mikusanyiko na maandamano na pia kivutio cha watalii huku ikiwa ni sehemu pekee ya kijani ya umma iliyobakia kwenye mji wa Istanbul. Makumi ya watu wamejeruhiwa na wengine wengi kutiwa mbaroni katika vurugu hizo. 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO