Wednesday, June 19, 2013

WATU 60 WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA INDIA

Takriban Watu 60 wanahofia kupoteza maisha wengine maelfu wakiachwa bila makazi baada ya mvua kubwa kunyesha na kubomoa nyumba na kuharibu barabara kaskazini mwa India. Shughuli za uokoaji zimeanza Mamlaka ikitumia Helkopta za kijeshi kujaribu kuaokoa wakazi walionasa kutokana na Mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua zilizonyesha kwa zaidi ya siku tatu katika jimbo la Uttarakhand. Waziri anayeshughulika na majanga na uokoaji amesema kuwa wameshindwa kuthibitisha idadi ya Watu waliopoteza maisha kwa kuwa miundo mbinu ya Mawasiliano imeharibika .
 Picha za Televisheni zimeonesha Madaraja na nyumba zikianguka kisha kuzolewa na maji yenye kasi. Miundombinu ya Barabara imeharibiwa, huku ikiwaacha mamia ya waumini waliokuwa wakielekea kwenye nyumba ya kuabudu wakiwa katika hali ya sintofahamu. Katika maeneo mengine mvua zilizokuwa zimeendelea kunyesha zimesababisha zoezi la uokoaji kuwa gumu , huku Waokoaji kutoka kitengo cha taifa cha kupambana na Majanga nchini India wakisubiri kutekeleza jukumu hilo kwa njia ya anga. Mvua za masika nchini India, hutegemewa sana na Sekta ya Kilimo nchini humo mvua ambazo hunyesha kuanzia mwezi June mpaka mwezi Septemba zikisababisha mafuriko.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO