Habari kutoka mjini Mombasa, Pwani ya Kenya zinasema kuwa, mshukiwa mmoja wa ugaidi amepigwa risasi na kuuawa. Mshukiwa huyo alipigwa risasi baada ya kukataa kujisalimisha kwa polisi. Polisi wanasema wamefanikiwa kupata maguruneti na zaidi ya bunduki mbili zikiwa na risasi 200 nyumbani kwa mshukiwa huyo.
Mkuu wa polisi mjini humo, Aggrey Adoli amesema kuwa, mshukiwa alikuwa anapanga kufanya mashambulizi ya kigaidi mjini Mombasa na Nairobi.
Tukio hilo linakuja wiki moja baada ya watu sita kuuawa katika shambulizi la kigaidi lililofanya dhidi ya kanisa moja mjini Mombasa. Polisi wamekuwa wakiwalaumu wapiganaji wa kundi la al-Shabaab kwa kufanya mashambulizi kama haya mara kwa mara nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO