Naibu Waziri Mkuu wa Uturuki, Bulent Arinc ametishia kwamba huenda serikali ikatumia jeshi kuzima maandamano yanayoendelea nchini humo kwa wiki ya pili mtawalia.
Tishio hilo la serikali limetolewa huku vyama viwili vya wafanyakazi vikifanya mgomo wa siku moja kupinga jinsi polisi wanavyotumia nguvu kupita kiasi katika kukabiliana na waandamanaji. Muungano wa madaktari na ule wa wahandisi kwa pamoja imetaka serikali kuheshimu uhuru wa kuandamana na kujieleza. Waandamanaji wanapinga mpango wa serikali wa kujenga majumba kwenye bustani mashuhuri ya Gezi mjini Istambul.
Waziri Mkuu, Recep Tayyip Erdogan amesema wanaoandamana hawana nia njema na kwamba wanatumiwa na wanasiasa wa upinzani ili kuivuruga serikali yake. Takriban watu 5 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa tangu kuanza maandamano hayo majuma mawili yaliyopita.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO