Monday, June 17, 2013

WAMISRI WAPINGA KAULI YA MURSI JUUYA SYRIA

Wananchi wa Misri wamekosoa vikali matamshi ya Rais Muhammad Mursi wa nchi hiyo kuhusiana na Syria na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon. Duru za habari nchini Misri zinaarifu kuwa, wananchi wa nchi hiyo wamekosoa matamshi ya hivi karibuni ya rais huyo kwa kuishambulia Harakati ya Hizbullah na hatua yake ya kukata uhusiano na serikali ya Damascus. Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Rais Muhammad Mursi alitangaza kuwa nchi yake imekata kabisa uhusiano wa kidiplomasia na serikali ya Syria na kuzitaka nchi za Magharibi kuanzisha eneo la marufuku ya kupaa ndege nchini humo. Maneno hayo ya Rais Mursi yameakisiwa sana nchini humo hasa kwa kuzingatia kuwa, yanaunga mkono njama za Marekani dhidi ya taifa na watu wa Syria. Ukosowaji huo haukufanywa na wananchi wa Misri pekee, bali hata baadhi ya majenerali wa jeshi la nchi hiyo nao wameyataja maneno ya rais huyo kuwa yasiyofaa. Kabla ya hapo kwa mara kadhaa jeshi la Misri lilikuwa likipinga uungaji mkono wa serikali ya Cairo kwa waasi wa Syria.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO