Saturday, June 08, 2013

OBAMA ATOA MWITO KUANZISHA USHIRIKIANO MPYA NA CHINA

Rais Obama ametoa mwito wa kuanzisha ruwaza mpya  ya ushirikiano baina ya Marekani na China.
Obama alitoa mwito huo, alipomkaribisha Rais wa China Xi Jinping anaefanya ziara ya siku mbili nchini  Marekani. Rais Obama amekiri kwamba katika muundo wa sasa wa ushirikiano baina ya Marekani na China pana sehemu kadhaa za mivutano, ikiwa pamoja na katika nyanja za vita vya mtandao wa komputa katika   biashara.
Hata hivyo Obama amesema Marekani na China zinaweza kushirikiana katika mambo mengi.
Kwa upande wake Rais wa China  Xi Jinping amesema mazungumzo yake na Rais Obama ni mwanzo mpya wa kihistoria . Ameeleza kwamba kukutana kwake na Rais Obama muda mfupi tu baada ya kuwa Rais wa China kunathibitisha umuhimu wa uhusiano baina ya China  na Marekani.         

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO