Saturday, June 08, 2013

RUSSIA KUPELEKA ASKARI WAKE MILIMA YA GOLAN

Rais Vladmir Putin wa Russia ametangaza kuwa tayari serikali ya Moscow kupeleka askari wa kulinda amani katika milima ya Golan, kuchukua nafasi ya vikosi vya Austria. Serikali ya Austria imetangaza kuvitoa vikosi vyake katika eneo la milima ya Golan, kwa kuhofia usalama wa askari wake. Rais Putin amesisitiza kuwa, kuna udharura mkubwa wa kuwepo askari wa kulinda amani katika eneo hilo kutoka na hali tete iliyoko kati ya Syria na utawala wa Kizayuni wa Israel. Baada ya kujiri mapigano karibu na maeneo ya milima ya Golan, mara kadhaa makundi ya kigaidi yamekuwa yakiwakamata mateka askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa katika eneo hilo. Vikosi vya Umoja wa Mataifa vilipelekwa katika eneo la milima ya Golan mwaka 1974 kwa lengo la kuhifadhi usitishaji mapigano kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na Syria. Kabla ya Austria, Japan na Ukraine zilishaondoa  wanajeshi wake katika eneo la milima ya Golan ya Syria inayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO