Baada ya miezi kadhaa ya mvutano, baina yao nchi mbili za Korea zimekubliana kuyaanzisha tena mazungumzo kwa mara ya kwanza baada ya muda wa zaidi ya miaka miwili.
Kwa mujibu wa wizara inayoshughulikia masuala ya kuungana tena, wajumbe wa nchi hizo watakutana kwenye mji wa mpakani, Panmunjom.
Wajumbe hao watautayarisha mkutano wa ngazi ya mawaziri unaotarajiwa kufanyika Jumatano ijayo katika mji mkuu wa Korea ya Kusini, Seoul.
Mkutano rasmi baina ya nchi mbili za Korea ulifanyika kwa mara ya mwisho mnamo mwezi wa Februari miaka miwili iliyopita.
Korea ya Kaskazini ilipendekeza hapo juzi kufanyika mazungumzo hayo juu ya kuianzisha tena miradi ya kiuchumi ya pamoja.
Katika hatua nyingine ya kupunguza mvutano baina ya nchi mbili za Korea, Korea ya Kaskazini imeyaanzisha tena mawasiliano ya simu na shirika la Msalaba Mwekundu la Korea ya kusini .
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO