Polisi wamefanya misako katika majimbo matatu ya Ujerumani ikiwa ni sehemu ya kinachoeleweka kuwa uchunguzi wa mipango ya kufanyika mashambulio ya kigaidi.
Polisi hao walifanya misako katika majimbo ya Baden Württemberg,Bavaria na Saxony.
Kwa mujibu wa taarifa, watu wanaotuhumiwa kuwa waislamu wenye itikadi kali,walipanga kufanya mashambulio kwa kutumia ndege za sanamu zilizojazwa mabomu ambayo yangeliweza kufyatuliwa kutokea mbali.
Baadhi ya ripoti zimesema kuwa watuhumiwa hao wana nasaba ya Kitunisia na walikuwa wanasomea uhandisi kwenye chuo kikuu cha Stuttgart katika jimbo la kusini mwa Ujerumani ,la Baden Württemberg.
Misako ya polisi inafuatia tahadhari zilizotolewa na idara ya Ujerumani ya upelelezi wa ndani, kuwa Ujerumani imekuwa lengo kuu la magaidi wa kiislamu wenye itikadi kali.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO