Sunday, June 16, 2013

POLISI WAIVUNJA KAMBI YA WAANDAMANAJI

Polisi wa Uturuki wametumia nguvu kuivunjilia mbali kambi ya waandamanaji katika bustani ya Gezi mjini Istanbul.
Kwanza walitumia maji ya kuwasha na gesi ya kutoa machozi kuwafurusha maalfu ya waandamanaji.
Baada ya hapo halmashari ya mji ilipeleka matingatinga na magari ya kuzolea taka ili kuondoa kila kitu kilichoachwa na watu ambao wamekuwa wanaandamana kwa muda wa zaidi ya wiki mbili.
Kundi linaloongoza maandamano limesema , mamia ya waandamanaji walijeruhiwa kutokana na polisi kutumia nguvu kupita kiasi.
Kundi hilo la mshikamano wa bustani ya Taksim limeiita hatua ya polisi kuwa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO