Saturday, June 01, 2013

SERIKALI YA JAMHURI YA A/KATI YATAKA KUKAMATWA BOZIZE

Serikali ya jamhuri ya afrika ya kati imetoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa rais wa zamani wa taifa hilo, Francois Bozize ambaye aliondolewa madarakani na waasi kwenye mapinduzi ya mwezi March mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwendesha mashtaka mkuu wa Serikali, hati hiyo imetolewa kutokana na makosa ambayo rais Bozize aliyatenda wakati akiwa madarakani ambapo ni pamoja na makosa ya ukiukaji wa haki za binadamu.
Alain Tolmo ameongeza kuwa hati hiyo ilitolewa toka mwezi May mwaka huu kwakuwa makosa mengi ambayo wanamshtaki nayo rais Bozize yanaangakia katika mkataba wa kimataifa wa mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC. Bozize ambaye alikimbia nchi yake punde baada ya mapinduzi, anashatakiwa pamoja na matendo ya kukiuka haki za binadamu, pia maujai ya watu 22 na mauaji ya pamoja ya rais 119.
Kiongozi huyo pia anatuhumiwa na Serikali mpya ya waasi wa Seleka, ya kwamba wakati wa utawala wake aliamrisha kukamatwa bila ya makosa kwa wananchi waliokuwa wakipinga utawala wake pamoja na kuwabomolea nyumba wananchi zaidi elfu 4. Kwa upande wa mahakama ya ICC kupitia msemaji wake imesema kuwa haijatoa hati yoyote ya kukamatwa kwa rais Bozize.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO