Watu watatu wameuwawa nchini Syria baada ya Jeshi la nchi hiyo kufanya mashambulizi ya angani mjini Homs. Kulingana na shirika la kutetea haki za binaadamu nchini humo, vikosi vya serikali bado vinaendelea na juhudi za kudhibiti mikoa ambayo inashikiliwa na waasi.
Mkurugenzi wa shirika hilo Rami Abdel Rahman amesema watu hao waliouwawa ni mwanamke mmoja na watoto wawili na mamia ya watu wameachwa na majeraha tangu kuanza kwa mashambulizi ya angani kutoka kwa vikosi vya serikali hapo jana. Rami Abdel Rahman amesema jeshi kwa sasa linajaribu kuingia mjini Khaldiyeh lakini bado hawajafanikiwa.
Homs ambao ni mji wa tatu kwa ukubwa nchini Syria ni miongoni mwa miji ya mwanzo kujiunga na uasi dhidi ya Rais Bashar Al Assad zaidi ya miaka miwili iliopita.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watoto 6000 ni miongoni mwa watu 93,000 waliouwawa hadi sasa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO