Polisi wametumia mabomu ya kutoa machozi na maji kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wameweka vizuizi karibu na majengo ya bunge la Uturuki.Waandamanaji hao wamekataa kuondoka kutoka mji wa Istanbul wakati maandamano hayo yakidumu kwa zaidi ya wiki mbili sasa. Makabiliano hayo ya hivi punde kati ya polisi na waandamanaji hao yanakuja saa chache baada ya serikali ya Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuwaomba wawakilishi wa waandamanaji hao kuwarai mamia ya wenzao waliokita kambi katika bustani ya Gezi kuondoka.Erdogan ameahidi kuruhusu mahakama na ikiwezekana kura ya maoni kuamua hatma ya mpango wa ujenzi katika bustani ya Gezi iliyozua maandamano hayo makubwa dhidi ya serikali ambayo hayajashuhudiwa nchini humo kwa miongo kadhaa.Wafuasi wa Erdogan wanapanga maandamano leo katika miji ya Ankara na Istanbul kumuunga mkono.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO