Kampuni za Facebook na Microsoft zimesema kuwa baada ya mazungumzo na maafisa wa shirika la kitaifa la upelelezi la Marekani wamepewa ruhusa ya kufichua kwa kiasi fulani kuhusu maagizo ya serikali ya Marekani kuzitaka kampuni hizo kufichua data za watumiaji wa mitandao hiyo. Tangazo hilo linakuja wiki moja baada ya mfanyakazi wa zamani wa shirika hilo la upelelezi la Marekani Edward Snowden kufichua kuwa Marekani inadukua data za watumiaji wa mitandao na simu.Facebook,Microsoft na Google ambao ni mahasimu katika biashara yamekuja pamoja kuishinikiza serikali ya Rais Obama kulegeza sheria kuhusu maagizo hayo ya kufichua data.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO