Sudan imesema kuwa waasi wa Sudan Kusini walishambulia bomba la mafuta katika eneo lenye mafuta la Diffra siku ya Jumatano, na kusababisha mlipuko na moto kwa masaa kadhaa. Al Sawarmi Khalid msemaji wa jeshi la Sudan ameeleza kuwa, bomba hilo linalosafirisha maafuta hadi kwenye kiwanda cha Heglig limekarabatiwa na kuanza tena kufanya kazi. Khalid ameongeza kuwa, waasi wa JEM ndio waliofanya shambulizi hilo kutokea jimbo la Sudan Kusini na walisaidiwa na jeshi la nchi hiyo.
Sudan Kusini imeanusha madai hayo na msemaji wake Makol Arik amesema, hawawezi kufanya hivyo wakati ambapo wanahitajia mafuta yao kusafirishwa na Sudan. Nchi hizo mbili kwa muda mrefu zinatuhumiana kuwaunga mkono waasi wa upande wa pili na hivi karibuni Sudan ilitangaza kusimamisha usafirishaji wa mafuta ya Sudan Kusini kwa madai kwamba Juba inasaidia waasi dhidi yake ya Khartoum.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO