Wednesday, June 19, 2013

WATALIBAN WASHAMBULIA KAMBI YA JESHI

Kundi la wanamgambo la Taliban lakiri kuhusika na shambulizi nchini Afghanistani shambulio lililogharimu maisha ya Wanajeshi wanne wa Marekani, saa kadhaa baada ya Washington kusema kuwa itafanya mazungumzo na Wanamgambo juu ya kumaliza vita vilivyodumu kwa zaidi ya Muongo mmoja. Shambulio la Roketi lilipigwa katika kambi inayoongozwa na Vikosi vya Marekani, Bagram iliyo eneo la kaskazini mwa Mji wa Kabul.
Kabla ya Shambulizi hilo Rais wa marekani, Barrack Obama alikaribisha mazungumzo yaliyopangwa kufanyika nchini Qatar na kusema kuwa ni hatua muhimu. Wanamgambo wa Taliban walivunja mawasiliano na Marekani mwaka jana na wamekuwa wakikataa kufanya mazungumzo na Serikali ya Kabul. Hapo jana Majeshi ya NATO yalikabidhi jukumuu la kulinda usalama mikononi mwa Majeshi ya Afghanistani.
 Msemaji wa Taliban nchini Qatar, Mohammad Sohail Shaheen amethibitisha kabla ya shambulio la Bagram kuwa Taliban itaendelea kuishambulia Marekani nchini Afghanistani wakati mazungumzo yakiendelea. Rais Obama ametoa wito kwa kundi la Taliban kuvunja Mahusiano na Al- Qaeda, kuacha mashambulizi na kujikita katika kulinda Wanawake na Raia wasio na hatia, na kuonya kuwa Vikosi vya NATO vitaendelea na Mapambano dhidi ya Al Qaeda.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO