Makumi ya maelfu ya waandamananaji wamejitokeza katika miji mingi ya Uturuki na kupuuza wito wa Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan aliyewataka wasitishe maandamano. Serikali imesema 'imedhibiti' maandamano katika hali ambayo idadi kubwa zaidi ya waandamanaji ilikusanyika katika medani ya Taksim mjini Istanbul ambayo ni kitovu cha maandamano ya kitaifa ambayo yamekuwa yaliendelea uturuki kwa siku tisa sasa. Ghasia Uturuki zilianza kufuatia mpango wa serikali wa kuharibu bustani ya Gezi karibu na medani hiyo na badala yake kujenga maduka. Bustani ya Gezi imezoeleka kuwa eneo la mijumuiko, mikusanyiko na maandamano na pia kivutio cha watalii huku ikiwa ni sehemu pekee ya kijani ya umma iliyobakia kwenye mji wa Istanbul. Mamia ya watu wamejeruhiwa na wengine wengi kutiwa mbaroni katika vurugu hizo. Waandamananaji aidha wamelaani vikali msimamo wa Erdogan wa kuunga mkono magaidi wanaotaka kuiangusha serikali ya wananchi wa Syria. Waturuki sasa wanataka Waziri Mkuu Erdogan ajiuzulu na uchaguzi wa mapema kuitishwa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO