Sunday, June 09, 2013

WATU 30 WAUAA BENGHAZI LIBYA

Watu karibu 30 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mji wa mashariki mwa Libya wa Benghazi katika mapigano kati ya waandamanaji na wanamgambo wenye silaha. Maafisa wa Libya wamearifu kuwa, karibu waandamanaji 200 baadhi yao wakiwa na silaha jana walikusanyika katika makao makuu ya kundi la wanamgambo wanoajiita 'Brigadia ya Kujilinda ya Libya' mjini Benghazi wakitaka kupigwa marufuku makundi yenye silaha kujiunga na jeshi. Malalamiko hayo yaligeuka kuwa mapigano ambapo watu karibu 30 waliuawa na mwengine 60 kujeruhiwa. Tangu kuangushwa utawala wa dikteta Muammar Gaddafi mwaka 2011, serikali ya Libya imekuwa ikijitahidi kupambana na makundi yenye silaha kama la Brigadia ya Kujilinda ya Libya ambalo linaundwa na wanamgambo waliopigana dhidi ya vikosi vitiifu kwa Gaddafi. Mapigano hayo yalimalizika baada ya kikosi maalum cha usalama kutuliza ghasia na kudhibiti eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO