Waziri mkuu wa Misri ameshutumu mauaji ya Waislamu wanne wa madhehebu ya Shia yaliyofanywa na kundi la Wasunni ambalo linajumuisha Wasalafi wenye msimamo mkali katika kijiji karibu na mji mkuu Cairo. Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu Hesham Kandil leo imesema kuwa anafuatilia kwa karibu uchunguzi kuhusu tukio hilo ili kuhakikisha kuwa wahusika wanaadhibiwa.
Misri ni nchi yenye waumini wengi wa madhehebbu ya Sunni ikiwa na idadi ndogo ya Washia. Kiasi ya asilimia 10 ya wakaazi milioni 90 wa nchi hiyo ni Wakristo. Shambulio hilo lililotokea jana Jumapili limekuja wiki moja baada ya viongozi kadha wa kundi la Salafi kuwakashifu Washia wakati wa mkutano uliohudhuriwa na rais wa nchi hiyo Mohammed Mursi. Mmoja wa viongozi hao wa kidini Mohammed Hassan , amemtaka Mursi kutofungua mpango wa Misri kwa washia, akisema kuwa hawaingii mahali bila ya kuleta ufisadi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO