Saturday, June 15, 2013

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA ASAINI MKATABA WA MTO NILE

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn ametia saini mkataba wa ugawanaji sawa wa maji ya Mto Nile miongoni mwa nchi unakopita mto huo. Bunge la Ethiopia limempa idhidi Waziri Mkuu kusaini mkataba huo, hatua inayotarajiwa kuongeza msuguano na Misri ambayo kwa sasa inapinga mipango ya Addis Ababa ya kujenga bwawa kubwa ili kunufauka na maji ya mto huo. Mkataba huo unachukua nafasi ya mkataba wa zama za ukoloni ambapo Misri na Sudan ndizo zilizopewa haki kubwa katika utumiaji wa maji ya Mto Nile. Misri inatarajiwa kutuma ujumbe wa ngazi za juu utakaoongozwa na Waziri Mkuu, Hisham Qandil nchini Ethiopia ili kuishawishi Addis Ababa asimamishe ujenzi wa bwawa la Renaissance. Rais Muhammad Mursi ametishia kwamba nchi yake iko tayari hata kutumia nguvu ili kuzuia Ethiopia kujenga bwawa hilo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO