Saturday, June 15, 2013

WAPALESTINA WAILAANI ISRAEL KWA UJENZI WA VITONGOJI

Waziri Mkuu mpya wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Rami Hamdallah amelaani mpango wa utawala haramu wa Israel wa kutaka kujenga vitongoji vipya katika ardhi za Wapalistina unazozikalia kwa mabavu. Rami amesema hatua kama hiyo itaendelea kudidimiza matumaini ya kuwa na madola mawili kama njia ya kutatua kadhia ya Palestina. Makundi ya kijamii ya Palestina yamesema yataandamana kupinga vikali hatua hiyo. Hii ni katika hali ambayo, baraza la walowezi wa Kizayuni limemtaka Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Israel, Benjamin Netanyahu aidhinishe ujenzi wa nyumba 550 katika eneo la Bruchin. Kuendelea ujenzi wa vitongoji vya Wazayuni katika ardhi za Wapalestina kumelaaniwa na Umoja wa Mataifa pamoja na taasisi zingine muhimu za kimataifa lakini utawala huo haramu umeendelea kutia pamba masikioni kutokana na uungaji mkono unaopata kutoka kwa Marekani na waitifaki wake.  

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO