Waturuki waishio nchini Ujerumani na Uholanzi, wametangaza uungaji wao mkono kwa waandamanaji nchini Uturuki. Waandamanaji hao wamekusanyika mbele ya ubalozi wa Uturuki mjini Berlin, Ujerumani huku wakitangaza kuyaunga mkono maandamano yaliyoenea nchini nzima huko Uturuki. Mmoja wa waandamanaji hao huko Berlin amesikika akisema kama ninavyomnukuu: “Tunachotaka sisi ni kukomeshwa ukandamizaji wa polisi na kujiuzulu serikali ya Ankara” mwisho wa kunukuu. Wakati huo huo mamia ya waandamanaji katika mji mkuu wa Uholanzi, Amsterdam wamekusanyika katika medani moja ya mji huo na kutoa nara za kuwaunga mkono raia wenzao wa Uturuki dhidi ya serikali ya Ankara. Aidha waandamanaji, wamelaani kile walichosema kuwa ni, ukandamizaji uliozidi mipaka wa haki za binaadamu nchini humo. Waandamanaji hao wa Uholanzi wamesema kuwa, wananchi wa Uturuki wanakandamizwa sana na serikali ya Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan. Maandamano ya kupinga serikali, yameendelea kushuhudiwa karibu katika miji yote ya nchi hiyo kwa siku ya 3 mfululizo, hali iliyomfanya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Daoud Oglokutangaza kuwa, maandamano na machafuko hayo yanaharibu jina la Uturuki duniani.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO